Connect with us

East Africa

Susumila Feat Mbosso – Sonona lyrics

Published

on

 (Mocco)

Siku moja moja
Ukipata nafasi tukumbukane
Nitalipa bodaboda
Acha na mwendo kasi usijibanebane
Aha, ewe binti maringo
Sijui wanisikia
Pendo lako nicheze bingo
Huenda nikajishindia
Mwenzako bado niko single
Pendo limenichachia Aaah
Uwe suka niwe tingo Niyoyoe abiria

Nafsi unainyong'onyeza (Aaah)
Nahisi la moyo shambulio (Aaah)
Nifanye chipsi chombeza (Aaah) J
apo unionje onje mwenzio (Aaah)
Penzi linanilegeza
Sonona, sonona

Eti lini utapata nafasi?
Sonona, sonona
Oooh beiby yoyo, nambie basi
Sonona, sonona
Nafsi nyonge, naishi kwa wasi wasi
Sonona, sonona
Beba wangu moyo, mwepesi ka karatasi
Sonona, sonona

Mwaga wino
Wa kalamu ya penzi langu
Chimba shimo
Unizike kabla ya siku yangu
Hakuna asiyejua
Matatizo ya moyo ukipenda
Unanifanya mwanasesere Kunichezesha
Mi muoga macho usoni
Nisijeshikwa na kwikwi kimasihara
Sema niandae vipopconi
Unyonye na vipipi vya duara

Nafsi unainyong'onyeza (Aaah)
Nahisi la moyo shambulio (Aaah)
Nifanye chipsi chombeza (Aaah)
Japo unionje onje mwenzio (Aaah)
Penzi linanilegeza
Sonona, sonona

Eti lini utapata nafasi?
Sonona, sonona
Oooh beiby yoyo, nambie basi
Sonona, sonona
Nafsi nyonge, naishi kwa wasi wasi
Sonona, sonona
Beba wangu moyo, mwepesi ka karatasi
Sonona, sonona

Uje (Uje)
Uje beiby (Uje)
Uje Mombasa wakuone
Uje (Uje)
Uje darling (Uje)
Uje Nairobi wakuone
Uje (Uje)
Uje beiby (Uje)
Uje Dar es
Salaam wakuone
Uje, uje beiby
001 akuone

MoccoGenius!

Continue Reading
Advertisement
Click to comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Trending 🔥🔥