Connect with us

East Africa

Mbosso – Haijakaa Sawa Lyrics

Published

on

 Verse One
Sasa unanuna nini?
Au unadhani hata mimi napenda
Nishazichoka na mimi
Mboga za majani kila siku mrenda

Siko juu siko chini
Niko nusu Sadoo
Si wa kumi si sabini
Ngoma ngumu bado

Kama ibada naswali sana
Usiku wa manane tena nafunga na Suna
Mambo bado bado mwana wale
Naona yanazidi kuguma

Nikirudi na hasira hasira
Nizoee
Mambo magumu bado bila bila
Niombee

Nikirudi na hasira hasira
Nizoee
Mambo magumu bado bila bila
Niombee

Chorus
Halijakaa sawa
Nivumilie ipo siku tutapata
Halijakaa sawa
Shida na dhiki zitakwisha baby

Halijakaa sawa
Kuchana kope make up utapaka
Halijakaa sawa
Tutabadili mboga kuku kwa manyama

Verse Two
Chochea kuni kipenzi changu
Asubuhi tumbo likikuming’inya
Pokea kidogo changu
Tunywe chai na mkate wa ku mimina

Akili ikichoka riziki nikikosa
Najua kwako nitajiliwaza
Kama makosa nivute chumbani
Kununa nuna unajilemaza

Ustahimilivu mnao wachache mno
Jua shida rafiki wa mbivu
Baada ya dhiki mavuno
Kila jema lina maumivuu
Na kwenye waliomo tumo

Yarabi salama tupe tulivu
Penzi lisifike kikomo
Iyeee yeee eee
Nikirudi na hasira hasira
Nizoee

Mambo magumu bado bila bila
Niombee
Nikirudi na hasira hasira
Nizoee
Mambo magumu bado bila bila
Niombee

Chorus
Halijakaa sawa
Nivumilie ipo siku tutapata
Halijakaa sawa
Shida na dhiki zitakwisha baby

Halijakaa sawa
Kuchana kope make up utapaka
Halijakaa sawa
Tutabadili mboga kuku kwa manyama

Continue Reading
Advertisement
Click to comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Trending 🔥🔥